LIGHTNING WALLET lighting network ni mfumo rafiki unaowezesha uharaka,unafuu wa gharama za miamala ya BITCOIN, na sifa kemkem tulizoziona kweny majarida yaliyopita kuhusu lighting network. Na ili kufaidi haya na kufanya miamala katika mfumo wa lightning network inahitajika pochi ya lighting(lighting wallet). Lighting wallet ni nini? Hii ni programu yenye aplikesheni inayokuwezesha kutuma,kupokea na kuhifadhi sarafu bitcoin Kwa kiwango cha satoshi (satoshi ni kiwango kidogo cha bitcoin kwa mfano centi kwenye shilingi). Aina mbili kuu za pochii ambazo ni;- 1.Custodial wallets; hizi n pochi ambazo usimamizi wa funguo binafsi upo kwenye mamlaka za pochi husika. Zina rahisisha kutuma na kupokea sarafu mtandao. Pia uzuri ni kuwa ikitokea umesahau fungua za pochi yako unaweza kuomba funguo mpya Kwa wamiliki wa pochi kupitia e-mail na utakuwa hujapoteza sarafu zako zilizokuwa kwenye pochi yako . Kwa sifa hii inawasaidia watu wanaoanza safari ya sarafu mtandao(Bitcoin). Mfano ni wallet of SATOSHI, blue wallet nk 2. Non custodial; hizi ni pochi ambazo usimamizi wa funguo binafsi upo kwenye mamlaka ya mtumiaji mwenyewe. Hizi hutumiwa na wazoefu zaidi katika sarafu mtandao. Na ikitokea umesahau password au kupoteza funguo binafsi bas unakuwa huwez kuzipata tena na kusababisha kupoteza sarafu zako kabisa. Mfano ni Muun, Phoenix nk
Hizi Aina mbili zinaanguka katka makundi mawil;- mobile wallets(hot) na hardware wallets (cold) 1.Mobile wallets hot.. hizi ni pochi ambazo zinaweza kufanya kazi kwa kuwepo interneti na hufanya kazi kwenye vifaa kama simu, computer na browsers. Faida ya hizi ni kuwa mda wowote utaweza kutumia sarafu zako. Pia kubadili upate cash au kufanya malipo ya sarafu mtandao.🎯Hizi zinafaa Sana kwa watu wanaozitumia sarafu zao kwenye matunizi ya kila siku. 2. Hardware wallets cold hizi ni pochi ambazo hutunza sarafu mtandao bitcoin Kwa muda mrefu katika vifaa maalumu . Mtu anapohitaji sarafu zake huziamishia kwenye mobile wallets ndipo utaweza kutumia.🎯Hizi zinafaa kwa watu wanaotunza sarafu mtandao zao kwa muda mrefu bila kuzitumia