Maisha yetu chimbuko lake ni ardhini, tumetoka ardhini sisi, viumbe na mimea tunayokula na maji tunayokunywa, vyote vina asili ya ardhini.

Ardhini kuna madini, chumvichumvi, antibiotics, antifugal na anti-viral chemicals. Udongo ni maisha na maisha ni udogo.

Je, unazifahamu faida za kutembea bila ya viatu, kushika na kuubusu udongo/ardhi?

Mitume yoote, manabii wote, wagunduzi na wafumbuzi woote wenye hadhi ya Newton, Socrates, Avogadro, Eisten, Boyle, Archimedes na nk, mababu zetu, maaskofu, mapope, masheikh, walioandika vitabu vya dini kama Bibilia na Msahafu na wengine wengi ambao waliofanya mambo ya maana hapa duniani wote walikuwa mara nyingi wakitembea kwa miguu ardhini, kushika udogo na kuibusu ardhi kwa nyakati tofauti.

Magonjwa mengi kuanzia vidonda hadi upunguvu wa damu vilikuwa vikitibiwa kwa udogo. Hadi sasa wanyama, wadudu, ndege, samaki na mimea yote vinajipakaa mchanga/mchanga kwa sababu mbalimbali za kiafya kama sehemu ya matibabu.

Kwa binadamu:

Kutembea bila viatu

1. kunavuta sumu za mwilini kwenda ardhini kupitia vinyweleo/ndugu ndogo zilizoko kwenye ngozi. Uvutano wa dunia na mwili (gravitational forces), osmosis na sweating vinasaidia jambo hili kutokea.

2. mchanga unavuta harufu mbaya ya mwilini na kupotelea ardhini. mtu anayetembea peku hasumbuliwi na fangasi wala harufu mbaya ya soksi wala jasho baya.

3. Mpapaso(massage) kati ya ardhini na nyao za miguu unasababisha msisimko wa tissue zote (misuli, neva, ubongo, mimeng'enyo na vichocheo mabali mbali vya mwili mzima kuimarika na kuwa madhubuti sana. Hii inasababisha voiungo vyote hivi kufanya kazi kwa usahihi wake (use and disuse).

4. Kutembea peku ardhini (sio kwenye tiles au lami) kunasawazisha uzalishaji na utoaji wa hormones mwilini, hali hii inaondoa msongo wa mawazo (stress free) hivyo kumfanya mtu awe mwenye furaha mara zote na kuweza kupata usingizi wa kweli na halisia. Usingizi wa aina hii unazifanya ndoto za mtu ziwe za kweli na zenye maana.

5. Ardhi inaponyesha majeraha na michubuko kwenye ngozi, babu zetu walitibu vidonda kwa kuviweka mchanga tu basi. wakati mwingine udongo ni chakula, mama zetu wajawazito wanakula kuuongeza madini ya damu (iron) na yako makabila bila yanachanganya usali na udogo na kuwa sehemu ya chakula cha kawaida.

6. Vijidudu vya ardhini vikiingia mwilini kwa kiwango kidogo vinasababisha kinga kubwa ya mwili dhidi ya magonywa mbalimabli.

7. Kutembea bila viatu kwenye ardhi hasa ya moto wakati wa jua husaidia mzunguuko wa damu (perfusion) kwenye viungo vyote vya mwili, hivyo kuongeza uwezekano wa kuepula kupata magonjwa ya figo, pressure, kisukali.

8. Kutembea peku ardhini kunakufanya uonje uhalisia wako wa kuwepo duniani.

9. Kutembea ardhini kunajenga tabia ya kuwa makini na muangalifu, bila hivyo unaweza kujikwaa, kuungua, kuchomwa na miba na misumali, kuumwa na wadudu kama nyoka na nge. Hivyo kuwa makini kunakuwa sehemu ya maisha yako.

10. Ukifa hutakuwa mgeni sana kaburini, hahahaha!

Hatari za kutembea kwa miguu ni kama kujikwaa, minyoo ya safura, kugongwa na nyoka, funza, na mavumbi miguuni.

Vua viatu tembea japo kwenye bustani yako kuanzia sasa, utaona namna Mungu atakavyokutumia kwa mambo mengi. Utaona hata furaha yako itakavyoongezeka bila kuifahamu sababu, utaona namna kupanic kutakavyotawanyika kwako.