BINANCE YAPATA CEO MPYA

RICHARD TENG

Baada ya miaka sita madhubuti mwanzilishi na CEO Wakwanza wa Binance duniani Bw Chanpeng Zhao maarufu Kama CZ ameachia madaraka yake kutokana na tuhuma mbalimbali zilizomkumba katika harakati zake za kupambania maendeleo ya Blockchain na sarafu Mtandao

Ni dhahiri shahiri kuwa Mwekezaji huyu na mwanzilishi wa Binance mekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa watu wote wanapata huduma sawa katika masoko ya kifedha yanyohusisha sarafu za kidigitali katika mazingira salama

Niukweli kwamba Binance imekuwa kwa kasi Sana Ndani ya miaka sita ya uongozi wa CEO CZ kutokana na mifumo mizuri aliyoanzisha na kusimamia ya utoaji huduma kote duniani Bila kujali kipato Cha mtu

Watumiaji wa $Sarafu za Kidigitali ulimwenguni hasa walio mrengwa wa kulia wanalihesabu hili Kama Pigo katika Vita ya kutafuta uhuru wa Kifedha ijapokuwa haimanishi kuwa Ni mwisho wa Vita lakini hii inaleta sura Nyingine katika Hatamu ya Vita hivi vya biashara za kidigitali pamoja na fundomuunganiko

Serekali ya Marekani ndiyo Kinara wa Vita hii katika mataifa yote yanayopambana na Fundomuunganiko kwani mfumo huu hudhibiti mianya yote ya unyanyasaji na ufedhuli katika mifumo ya Kibiashara

Ni dhahiri kwamba Vita ndio vimeanza na Kitendo Cha kumtuhumu Bw Zhao inaamsha tu wale wataalam wengine kuanza kutengeneza mifumo madhubuti zaidi kwani hii inatudhihirishia kwamba Kama mwanzilishi wa Bitcoin angejulikana asingeweza kuachwa salama Hadi leo.

Kwa hakika Ni Matumaini yangu kwamba Bw Richard Teng ataendeleza mapambano Haya pale CZ alipoishia kwani tunafahamu kuwa Ni kiongozi likwisha kuandaliwa kwa muda mrefu, uadilifu wake unatupa Matumaini kuwa Hata Kama Vita hivi hatavimaliza lakini atakuwa mstari wa mbele kwa jamii ya kimataifa kuwaonesha Namna ambayo #Cryptocurrency inapaswa kupewa nafasi katika masoko ya ulimwenguni kujipambanua ili kuruhusu mapinduzi ya kiuchumi kitaifa na Kimataifa