Watu Kutaka pesa za haraka na kwa pupa
(Tamaa)
Hili ni tatizo ni kubwa sana miongoni mwa vijana
wengi wa Tanzania na Africa kwa ujumla, utakuta
kijana akishapata uelewa kidogo juu ya bitcoin
anaanza kutafuta sehemu ya kuwekeza kwa haraka
pasipokuwa na uhakika juu ya usalama wa kampuni
hiyo ila anawekeza kwasababu tu ameambiwa
inalipa vizuri na yeye anataka pesa za haraka..
mwisho wa siku anajikuta kampuni hiyo inapotea
mtandaoni na anakula hasara na baadae na yeye
anaanza kuamini kuwa cryptocurrency ni utapeli au
wizi na baadae anakata tamaa juu ya crptocurrency
na kuwathibitishia watu wa jamii inayomzunguka
kuwa cryptocurrency sio salama, kumbe yeye ndio
alikurupuka na kufanya maamuzi yasiyo sahii pia
hakupata uelewa wa kutosha juu ya fursa hii.